Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es
Salaam.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John
Pombe Magufuli amemtembelea na kumpa pole waziri mkuu mstaafu Mh.Fredrick
Sumaye ambaye amelazwa kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya taifa ya
Muhimbili na kuelezea namna alivyofarijika kwa kutembelewa na rais.
Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Fredrick
Sumaye ametembelewa na rais Dr John Pombe Magufuli katika hospitali hiyo ya
taifa ya muhimbili alikolazwa kwa ajili ya matibabu na kuelezea namna
alivyofarijika kwa kutembelewa na kiongozi huyo mkuu wa nchi na kuongeza kuwa
hatua hiyo inaonesha namna rais anavyowajali raia wake bila ya ubaguzi wowote
wa kiitika wa kivyama.
Aidha akizungumzia kuhusu hali yake Mh.Sumaye
amesema hali yake inaendelea kuimarika kutokana na matibabu anayoyapata
hospitalini hapo na kwamba kwa sasa ana nafuu na anataraji kuruhusiwa kuondoka
hospitalini hapo kurejea nyumbani wakati wowote.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akimpa pole Mama Maria Nyerere kufatia kufiwa na Mkwe wake Bi
Leticia Nyerere aliyefariki huko nchini Marekani. Rais alikwenda nyumbani kwa
Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam kumpa pole Mama nyerere.
Katika hatua nyingine rais Dr.John Pombe Magufuli
ameitembelea na kuipa pole familia ya mwalimu Nyerere kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo chadema Leticia Nyerere aliyefariki dunia
wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Maryland nchini marekani,rais Magufuli
ameitaka familia hiyo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wao.
0 comments:
Post a Comment