Aliyekuwa mgombea urais Zanzibar na Katibu Mkuu wa
Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif
Hamad amesema kuwa kutokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea visiwani
humo usipopatiwa ufumbuzi maramoja na kulazimisha kuwa uchaguzi huo urudiwe
nidhahiri kuwa hatua hiyo inalazimisha kuwepo kwa hali ya machafuko visiwani
humo.
Kauli ya Maalim Seif imekuja muda mfupi wakati
akiongea na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kuwaeleza ni namna
gani hali ya kisiasa visiwani humo ilivyo na mazungumzo waliokuwa wakizungumza
walipofikia hadi hivi sasa.
Amesema hali ya kisiasa bado tete kwakuwa vikao 8
walivyo kaa hadi sasa vimekuwa vya matumaini bila maridhiano yakina na kufikia
muafaka ambao umekuwa ukisubiriwa kwa hamu na wananchi pamoja watu mbali mbali
viwani humo hali ambayo imekuwa ikizusha maswali yakuwa kwanini mazungumzo hayo
hayakamiliki kwa wakati.
Kutokana na hatua hiyo sasa amemtaka rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli kuongoza mazungumzo ya
kutatua mgogoro wa kisiasa unaoendelea visiwani humo kwa kufuata misingi ya
kikatiba na sheria baada ya mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea kati yake na Dr
Ali Mohamed Shein kwa kuwashirikisha marais wastaafu wa Zanzibar kutoonesha
kuzaa matunda.
Hata hivyo katika mazungumzo ya Maalim Seif juu ya
majadiliano hayo ya kutafuta muafaka amemshutumu Dr Ali Shein kwa kusema kuwa
hakua na nia njema na mazungumzo hayo na hivyo amepoteza sifa ya kuongoza
mazungumzo hayo,huku akisema anazo taarifa kuwa tume ya uchaguzi imepanga
kukutana January ili kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi huku wananchi wa Zanzibar
wakiwa wako taaban na wamekumbwa na fadhaa baada ya kuona maamuzi yao
yanakanyagwa bila muafaka.
Pia Maalim ameendelea kwenda mbali zaidi akisema
kuwa kamwe tume haina mamlaka ya kutengua matokeo bali ina mamlaka ya kurudia
kuhesabu kura hivyo jambo alilolifanya mwenyekiti wa tume Zanzibar Jecha Salim
Jecha alienda kinyume cha katiba kwa kufanya maamuzi bila kushirikiana na tume.
Katiba inasema "kila uamuzi wa tume ni lazima
uungwe mkono na wajumbe walio wengi". Anasema katiba imetumia neno
'Lazima' na mwenyekiti kwenda kinyume inafaa kuchukuliwa hatua,alisema Seif.
Ingawa mwenyekiti aliitisha kikao kuhalalisha
maamuzi yake bado tume haikuwa na mamlaka ya kuhalalisha maamuzi ya kufuta
uchaguzi uliokamilika na Tamko la mwenyekiti lilisema anafuta uchaguzi na
matokeo yake yote hata hivyo tangazo rasmi lilisema anafuta matokeo ya uchaguzi.
Vifungu vya katiba vilivyonukuliwa, vimenukuliwa kwa
ubabaishaji kuhalalisha uwezo wa tume kufututa matokeo kifungu cha 34 kimeweka
utaratibu wa kufunga kituo ikitokea dosari,sheria imetoa fursa ya wazi kwa
mwenye malalamiko na kwa mujibu wa sheria hakuna malalamiko yaliyowasilishwa
mbele ya tume.
Tangu uchaguzi wa vyama vingi zianze zimekuwa
zimekumbwa na kasoro ukiwemo wa mwaka 2000 uliolazimu vituo 16 kurejea uchaguzi
Zanzibar, hivi kweli uchaguzi wa 2015 ulizidi kasoro za mwaka 2000.
Maalim amesema Tume haipaswi kupewa maagizo na chama
chochote cha siasa au chombo chochote, ni dhahiri maamuzi ya mwenyekiti
yalikuwa ya maagizo kama alivyowaeleza wenzake.
Athari za kufutwa kwa uchaguzi kumepelekea athari
kadha za kikatiba, mgogoro mkubwa wa kikatiba na kisheria.
Imepelekea Zanzibar kuwa na mgogoro kwa Rais aliyeko
madarakani, washauri wametumia tafsiri isiyo sahihi ya kikatiba hadi Rais mpya
atakapoapishwa.
Mpaka wa kifungu kinachorusu mpaka Rais ajae
atakapoapishwa ni kuwa muda wa Rais ni miaka mitano pekee na katiba haijaruhusu
muda wa miaka mitano uongezwe kiholela ila kwa masharti mazito ikiwemo vita na
Rais akaona ni muhimu kusitisha uchaguzi basi ataitisha baraza la wawakilishi
na linaweza kumuongezea muda usiozidi miezi sita.
Tafsiri isiyokuwa sahihi ina athari zifuatazo
Haujawekwa
muda maalum na katiba imeweka muda maalum kwa chaguzi zinazofutwa kisheria, kwa
maana hiyo hakuna ukomo mpaka uchaguzi utapoitishwa tena.
Tafsiri
hio haimpi fursa ya Rais kumuwajibisha mtu alienda kinyume cha katiba kwa
sababu imemnufaisha Rais. Tafsiri sahihi ni lazima Rais ashike madaraka ya
Urais na aachie nafasi hio baada ya miaka mitano isipokuwa kwa dharura zilizopo
kisheria.
Mgogoro wa kutokuwa na Rais halali tangu tarehe 3
November 2015 na ameendelea kufanya maamuzi makubwa ikiwemo ya uteuzi.
Hata hivyo inasikitisha kuona mimi nikikubali kuwa
kimya kipindi chote, inasikitisha kuona viongozi wa upande mwingine wakiongea
na kuwachanganya watu.
Magufuli pamoja na juhudi zote hakuacha kufitinishwa
kwa Balozi Seif Ali Iddi kusema eti Magufuli kasema turudi Zanzibar kukamilisha
taratibu za kurudia uchaguzi ilhali mimi hakuniambia.
Hadi jana ukiangalia tovuti ya uchaguzi Zanzibar
hadi jana inasema uchaguzi ulifanyika kwa amani nchi nzima.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa Zanzibar imepita
siasa za dhoruba na machafuko kwa miaka 50 ndio maana yeye kwa mwaka 2009
sambamba na na Rais mstaafu Karume walifikia maridhiano.
Wakati wa maswali kwa waandishi wa habari moja ya
Swali aliloulizwa na kutakiwa kulitolea ufafanuzi ni juu ya kuwa zipo taarifa
kuwa yeye sio Mzanzibari ambapo alisema kuwa “chaguzi tano nagombea urais na
hakuna mtu hata mmoja anaweka pingamizi, hata kumjibu ni kinyaa. Eti Zanzibar
vyama vya upinzani viruhusiwe kugombea nafasi zote kasoro Urais, wanaogopa
nini? Wote ni watanzania na wanaogombea kupitia vyama hivyo ni watanzania.
0 comments:
Post a Comment