WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekuatana na kufanya mazungumzo
na mabalozi wawili kutoka nchi za Qatar na Kuwait.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na mabalozi hao leo
,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amewashukuru
mabalozi hao kwa pongeza walizokuja kumpatia, pamoja na namna ambavyo nchi zao
zimekua zikisaidia Tanzania, ambapo ameahidi
kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na nchi zao.
Kwa upande wake, Balozi wa Qatar, Abdallah Jassim al
Maadad amesema Serikali yake itaendelea
kuisaidia Tanzania katika maeneo yote ambayo Qatar imepiga hatua kubwa na inaweza
kutoa msaada kwa Tanzania.
Amesema Quwait iko tayari kuwekeza nchini katika
sekta ya kilimo, kwa vile ardhi ya
Tanzania ni yenye rutuba na inafaa kwa shughuli za kilimo. Aidha, ametaja sekta
nyingine ambazo wangependa kuwekeza
ni pamoja na sekta ya uvuvi na viwanda.
Naye, Balozi wa Kuwait, Jasem Al Najem ambaye
amekuja kujitambulisha kwa Waziri Mkuu, amesema nchi yake kupitia ‘Kuwait fund’
iko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Balozi Najem,
pia ameshauri vituo vya uwekezaji vya Tanzania na Kuwait kufanya kazi kwa
ushirikiano zaidi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment