Mahakama kuu kitengo cha ardhi imetoa uamuzi na kuitaka
serikali kuacha kuendelea na zoezi lake la bomoabomoa kwa wananchi wa kata tatu
zilizopo wilaya ya Kinonondoni mpaka kesi ya msingi ikamilike.
Kesi hiyo ya kupinga bomoabomoa ya nyumba zilizojengwa
kinyume na taratibu ilifunguliwa na mbunge wa jimbo la kinondoni Maulid Mtulia
ambapo leo ilisogezwa mbele mpaka saa nane mchana kufuatia mabishano ya
kisheria kati ya mawakili wa serikali wanaoisimamia na wakili wa upande wa
walalamikaji.
Kesi hiyo namba 822 ya mwaka 2015 ilipangiwa jaji Penterine
Kente huku upande wa walalamikaji wakisimamiwa na wakili Abubakar Salim.
Lengo la mbunge Mtulia lakufungua kesi hiyo alisema kuwa
lengo si kufungua kesi kupinga ubomoaji wa wakazi wa mabondeni bali ni kutaka
wananchi hao watendewe haki ikiwa ni pamoja na kupewa viwanja walivyo ahidiwa.
“Maeneo mengine ya uongozi niliyokwenda najibiwa kuwa
viwanja walivyopewa baadhi na wengine kuahidiwa ilitokana na huruma ya Rais
mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete”Alisema.
Hata hivyo bomoabomoa katika maeneo ya mabondeni ilitazamiwa
kuzikumba zaidi ya nyumba 5000 kati ya hizo 114 tu ndizo zilizofanyiwa
tathmini.
0 comments:
Post a Comment