Na Asteria Muhozya.
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Muhongo amewataka Watendaji wa Wizara,Wakuu wa Taasisi
zilizochini yake na watumishi wote kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha
kwamba sekta za Nishati na Madini zinakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa
ikiwemo mabadiliko kiuchumi kupitia sekta hizo.
Profesa
Muhongo ameyasema hayo wakati wa kikao cha utambulisho wa viongozi
wapya wa Wizara kilichoshirikisha Menejimenti ya Wizara, Taasisi zilizo
chini yake zikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la
Maendeleo ya Petroli la Tanzania (TPDC), Wakala wa Ukaguzi wa Madini
(TMAA), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO), Chuo cha Madini Dodoma (MRI) na Watendaji kutoka Shirika la
Maendeleo la Taifa (NDC).
“Ni lazima tujitume,
hili ndio jukumu letu la kwanza. Wananchi wanataka umeme na wanataka
mabadiliko kupitia sekta za nishati na madini. Tufanye kazi kwa umoja na
uwazi kwasababu tumepewa fursa ya kuwatumikia wananchi hivyo ni lazima
tubadilike na mabadiliko ni lazima. Asiyeweza kuendana na kasi ya awamu
hii aondoke, hakuna atakayeonewa,” ameongeza Prof. Muhongo.
Prof
Muhongo aliongeza kuwa, kutokana na uzoefu wa viongozi hao na watendaji
wa Wizara na Taasisi anaamini kuwa yatakuwepo mabadiliko katika sekta
hizo kutokana na sifa zao kitaaluma na kiutendaji. “Wananchi wana imani
kubwa na uteuzi wetu na uwepo wetu katika wizara. Tufanye kazi kwa
manufaa ya Taifa”, amesema prof. Muhongo
Kwa upande wake
Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Justin Ntalikwa alieleza kuwa, uongozi
huo unatarajia kufanya kazi kwa uadilifu na umakini na kuongeza kuwa, “
jukumu lililo mbele yetu ni kubwa tunahitaji kufanya kazi kwa bidii
tukitumia uzoefu, wote kutekeleza majukumu yaliyo mbele yetu”,amesema
Profesa Ntalikwa.Naye, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia
masuala ya Madini, Profesa James Msofe, amesema kuwa, aanatarajia
kujifunza kwa kasi kubwa majukumu yake ili kuweza kufikia matarajio ya
wananchi na taifa.
Home
News
Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Muhongo awawekea mikakati mizito watumishi wa wizara hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment