Mchezaji wa Manchester Wayne Rooney ametwaa Tuzo ya
Mchezaji Bora wa Mwaka kwa 2015 nchini Uingereza akitetea tena tuzo ambayo pia
aliizoa mwaka 2014.
Hii ni mara ya 4 kwa Rooney kuzoa tuzo hii ambayo
hupigiwa kura na wanachama wa Chama cha Mashabiki wa Soka England.
Mapema Desemba Shirikisho la Soka la England
liliyaweka hadharani majina ya wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka
nchini humo.
Mwaka 2015 Rooney aliiongoza England kufuzu kuingia
fainali za Mataifa ya Ulaya, Euro 2016, ambazo zitachezwa huko Ufaransa mwezi
Juni huku akihakikisha England inashinda mechi zao zote 10 za kundi lao na
kuifungia Jumla ya mabao 5 kwa mwaka 2015 kwa England.
Kadhalika, alivunja rekodi ya Sir Bobby Charlton ya
Ufungaji Bora katika Historia ya England kwa kufunga mabao 51. Rekodi ambayo
iliwekwa na Charlton mwaka 1968 ilikuwa ya mabao 49.
Wachezaji wengine waliokuwa wanawania Tuzo hiyo ya
Mchezaji Bora wa Mwaka ni Joe Hart (Manchester City), Gary Cahill (Chelsea),
Raheem Sterling (Manchester City), na Harry Kane (Tottenham Hotspur).
Kura kwa Wagombea hawa zilipigwa mtandaoni na
upigaji ulifungwa Jumapili Januari 3.
Rooney alijizolea asilimia 37 ya kura, Harry Kane
30% na Hart 19%.
Kipa wa Stoke City Jack Butland ameshinda tuzo ya
Mchezaji Bora wa Mwaka ambaye hajazidi umri wa miaka 21.
Wawili hao watatunukiwa tuzo hizo kabla ya mechi ya
krafiki kati ya Ujerumani na Uingereza mjini Berlin 26 Machi.
0 comments:
Post a Comment