Wayne Rooney alifunga bao lake la kwanza katika
uwanja wa Anfield tangu mwaka 2005 na kuiwezesha timu yake kupanda katika
jedwali la ligi ya Uingereza.
Liverpool ilitawala mchezo huo huku mkwaju wa Emre
Can ukipanguliwa na kipa David De Gea.
Lakini Liverpool walilazimika kulipa makosa yao
wakati Wayne Rooney alipofunga mkwaju mzuri akiwa karibu na eneo la hatari
baada ya kichwa cha Marouane Fellaini kugonga mwamba wa goli.
Wageni hao ambao sasa wako katika nafasi ya tano
walikuwa hawajashambulia hata mkwaju mmoja katika lango la Liverpool hadi
mshambuliaji huyo wa Uingereza alipofunga bao hilo la ushindi.
Liverpool itasalia katika nafasi ya tisa ikiwa alama
sita nyuma ya Manchester United.
0 comments:
Post a Comment