TAARIFA KWA UMMA
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anakusudia kuyachukulia hatua Mashirika yanayoendesha shughuli zao kinyume cha Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005.
Mashirika hayo ni yale ambayo hayajawasilisha taarifa za mwaka kwa kipindi cha miaka miwili
pasipo kutoa sababu za msingi, kulipa ada ya mwaka au kuendesha shughuli za NGOs bila kusajiliwa chini ya Sheria ya NGOs.
Kwa taarifa hii, Mashirika husika yanatakiwa yawe yamerekebisha dosari tajwa ndani ya siku thelathini (30) kuanzia tarehe ya tangazo hili. Baada ya kipindi hicho, Msajili wa NGOs atayafutia usajili Mashirika ambayo yatakuwa hayajawasilisha taarifa na kuyachukulia hatua stahiki Mashirika yanayoendesha shughuli za NGOs bila ya usajili chini ya Sheria
husika.
Malipo yote ya ada yafanyike kupitia Benki ya NMB, NGO Account Na. 20110014074 na stakabadhi halali ya malipo itumwe kwa Msajili wa NGOs.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment