Klabu ya soka ya Liverpool hapo jana ilifanikiwa
kuifunga Stoke City bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya
michuano ya Capital One katika mchezo uliopigwa dimba la Brittania.
Bao pekee la Liverpool lilifungwa na mchezaji Jordon
Ibe katika dakika ya 37 kipindi cha kwanza ushindi ambao umempa furaha kocha
Jurgen Klopp na kumpa matumaini ya kutinga fainali ya michuano hiyo.
Iwapo watafanikiwa mechi ya marudiano, Liverpool
watakutana na mshindi wa nusufainali kati ya Everton au Manchester City, kwenye
fainali ambayo itachezewa uwanja wa Wembley.
Mechi ya kwanza ya nusufainali hiyo nyingine
itapigwa usiku wa leo ambapo Everton watakuwa nyumbani Goodson Park dhidi ya
Manchester City.
0 comments:
Post a Comment