Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu
ya TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta leo hii anatarajiwa kuwasili nchini
Nigeria kuhudhuria sherehe za utoaji wa tuzo kwa wachezaji bora barani Afrika
zitakazofanyika katika mji wa Abuja Alhamisi tarehe 7 Januari.
Mbwana Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa
Afrika kwa wachezaji wa ndani, huku pia akiwa mfungaji bora wa michuano ya Ligi
ya Mabingwa (CAF CL) baada ya kuifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao 8 na
kuibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo.
Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika
pamoja na mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba (Congo DR) na mshambuliaji
wa Etoile du Sahel Baghdad Boundjah (Algeria).
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Mwesigwa Selestine ameandamana na Samatta kuhudhuria sherehe hizo.
0 comments:
Post a Comment