Mawaziri watatu wakiongozwa na waziri wa nchi ofisi
ya rais Tamisemi utumishi na utawala bora wamefanya ziara katika machinjio ya
Vingunguti na kuwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wa umma kwa madai ya kuwepo
kwa ufisadi wa mali za umma.
George Simbachawene amewaongoza mawaziri wengine
ambao ni waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi Mwigulu Nchemba na Naibu waziri wa
afya Hamisi Kigwangala kufanya ziara katika machinjio hayo na kubaini matatizo
mbalimbali ikiwamo ukiukwaji wa taratibu za kulipia ushuru kwa wanyama ambapo
ilibainika idadi ya mbuzi ama ng'ombe wanaolipiwa ili kuingia katika machinjio
hayo nitofauti na vibali vinavyotolewa ambapo waziri wa mifugo alitoa mfano wa
jana alipofanya ziara ya kushtukiza usiku alikuta kuna vibali vya mbuzi miatatu
lakini idadi ya mbuzi waliyokuwepo ni zaidi ya miasita.
Naye waziri wa nchi ofisi ya rais Tamisemi George
Simbachawene alitaka kufanyika uchunguzi wa kina ili kubaini gharama za
kutengeneza vibanda vya kuwekea nyama ambavyo vilidaiwa kutengenezwa kwa
gharama ya shilingi milioni miamoja jamboa ambalo hakukubaliana nalo,huku naibu
waziri wa afya akimtaka waziri huyo wa Tamisemi kuondoka na daktari wa eneo
hilo kwa madai kushindwa kaza na kugubikwa na masauala ua ufujaji wa mali za
umma.
Mawaziri hao
waliondoka na kuacha maagizo ya baadhi ya watumishi waliyokuwepo zamu siku moja
kabla ya siku kuu ya Chrismass kuchunguzwa na wahusika wa ufisadi wa
kubatilisha vibali kuacha kazi wenyewe.
0 comments:
Post a Comment