Serikali imeiagiza kampuni ya JOYTI STRUCTURE
inayosimika nguzo za mradi mkubwa wa umeme kutoka Iringa mpaka Shinyanga katika
eneo la Dodoma Singida kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo ifikapo tarehe 20
mwezi April kama mkataba unavyoelekeza la sivyo atataifishiwa mali na
kufikishwa mahakamani kufuatia kusuasua kwa utekelezaji wake ambao umefikia
asilimia 30 tu mpaka sasa.
Mradi huo wa Msongo wa Kilovolt 400 maarufu kama
BACK BONE wenye urefu wa zaidi ya kilometa 670 unatarajiwa kuwa mkombozi wa
nishati ya umeme katika mikoa ya kanda ya kati na ziwa ambapo mkandarasi anaye
simika nguzo na kutandaza nyaya katika eneo la Dodoma-Singida tayari amelipwa
asilimia 65 ya fedha huku akitakiwa akabidhi kazi hiyo april 20 mwaka huu kama
mkataba kati yake na serikali unavyoelekeza.
Naibu waziri huyo pia akatembelea eneo la kikombo
ambapo kuna mgogoro kati ya Tanesco na kampuni hodhi la usimamizi wa rasilimali
za reli kuhusu malipo ya kupitisha nyaya za umeme juu ya reli katika eneo hilo
na kuagiza mgogoro huo kumalizwa mara moja ili wananchi wa kata hiyo waweze
kupata umeme
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa maeneo mbalimbali
ya Dodoma wakaomba kasi ya usambazaji wa umeme
hasa maeneo ya vijijini kupitia mradi wa REA kuongezeka ili wananchi
waweze kutumia nishati hiyo kuharakisha maendeleo na kujikwamua kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment