Watu sita wamefariki dunia huku wengine
ishirini na tano kujeruhiwa katika ajali
mbili tofauti za Barabarani zilizotokea januari mosi mwaka huu mkoani Morogoro
ambapo ajali moja imetokea eneo la Msosa mpakani mwa mkoa wa Iringa na Morogoro
na nyingine ikitokea eneo la Ngiloli
wilayani Gairo.
Akitoa tarifa ya ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa
wa Morogoro Lenard Paulo amesema ajali hiyo iliyotokea eneo la Msosa mpakani
mwa mkoa wa Iringa na Morogoro kwa kuhusisha gari lenye namba za usajil T 922
basi aina ya YOUTONG mali ya kampuni ya AL-HUSHOOM likiwa na abiria 42
likiendeshwa na Dereva Ramadhani Shomari likotokea jijini Dar-es-Salaam
kuelekea mkoani Mbeya na kusababisha vifo vya watu watatu akiwemo dereva wa
gari hilo huku majeruhi 16 wakilazwa katika hospitali ya mtandika mkoani
iringa.
Aidha kamanda Paulo akizungumzia ajali iliyotokea
eneo la Ngiloli wilayani Gairo amesema ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ya
toyota VITZ likitokea Tanga kuelekea mwanza kugongana na lori lililokuwa
likitokea kagera kuelekea dar es salamu na kusababisha vifo vitatu na majeruhi
watano ambao wamelazwa katika kituo cha afya Gairo .
Kwaupande wake NESI wa zamu katika hospitali ya mkoa
wa Morogoro Renrida Mwarabu amekiri kupokea vifo vitatu vilivyo tokana na ajali
iliyotokea maeneo ya msosa na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
cha Hosptali ya mkoa wa Morogoro huku mganga mkuu wa kituo cha afya gairo
Daktari Mustafa Kachele ameeleza maiti tatu za ajali ya Ngiloli Gairo
zimesafirishwa kwenda Nzega.
0 comments:
Post a Comment