Watanzania wametakiwa kuliombea taifa amani ili
liendelee kudumu katika hali ya utulivu upendo na mshikamano na kuepukana na
machafuko yanayoweza kutokana na
viongozi kushindwa kuongoza kwa haki na hivyo kujenga chuki miongoni mwa
wananchi wake.
Akitoa salamu za mwaka mpya kwa waumini wa kanisa
katoliki katika ibada ya uzinduzi wa parokia mpya ya mbarali askofu wa jimbo
katoliki la Iringa ambaye pia ni rais wa baraza la maaskofu katoliki nchini
TEC.Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa amesema watanzania wana kila sababu
ya kumshukuru mungu na kuendelea kuombea
viongozi wa nchi kutenda haki kwa watu wote ili amani iendelee kuwepo nchini.
Awali akisoma risala ya waumini wa parokia ya
mbarali katibu wa Parokia hiyo Bwana Francis Katuli amemshukuru askofu huyo wa
jimbo la Iringa kukubali kuigawa Parokia ya Rujewa na kuzaa parokia ya pili ya
mbarali kwa lengo la kurahisisha huduma za kiroho kwa waumini wake na kufanya
jimbo la iringa kufikisha idadi ya Parokia 38.
0 comments:
Post a Comment