Mahakama kuu kitengo cha ardhi imeahirisha kutoa
uamuzi kuhusu ombi la zuio ya bomoa bomoa ya wakazi wa kata tatu zilizopo
wilaya ya Kinonondoni mpaka saa nane mchana huu.
Kesi hiyo ya kupinga bomoa bomoa ya nyumba
zilizojengwa kinyume na taratibu ilifunguliwa na mbunge wa jimbo la kinondoni
Maulid Mtulia ambapo ilikuwa ianze kusikilizwa lakini ikakwama kufuatia
mabishano ya kisheria kati ya mawakili wa serikali wanaoisimamia na wakili wa upande
wa walalamikaji.
Kesi hiyo namba 822 ya mwaka 2015 inasikilizwa na
jaji Penterine Kente ambaye amesema atakuwa tayari kutoa uamuzi wa
mahakama saa nane mchana huu kutoka na maombi hayo kupelekwa chini
ya hati ya dharura.
Akiahirisha shauri hilo hapo jana jaji
Kente aliahidi kutoa uamuzi huo leo majira ya saa tano asubuhi
ambapo ameahirisha hadi saa nane mchana ambapo atatoa msimamo wa mahakama
kuhusu kusitisha zoezi la kubomoa maeneo ya mabondeni au lah.
0 comments:
Post a Comment