Nahodha wa zamani wa timu ya kriketi ya West Indies,
Chris Gayle amepigwa faini baada yake kumtongoza mwanahabari wakati wa
mahojiano ya moja kwa moja.
Gayle amepigwa faini ya dola 10,000 za Australia
(sawa na $7,200; £4,900) na klabu yake ya Melbourne Renegades inayocheza ligi
ya Big Bash.
Mchezaji huyo alimuuliza mwanahabari wa kipindi cha
Ten Sport Bi Mel McLaughlin kama wangeweza kwenda ‘date’ alipokuwa akihojiwa
wakati wa mechi ya ligi dhidi ya Hobart Hurricanes Jumatatu.
"Kuyatazama macho yako mara ya kwanza kabisa ni
jambo njema sana. Natumai tunaweza kuketi na kunywa kinywaji pamoja. Usione
haya mtoto," alimwambia.
Baadaye, amejitetea na kusema alikuwa tu anafanya
mzaha.
Chris Rogers, aliyekuwa nahodha wa Sydney Thunder
wakati Gayle alikuwa mchezaji wa kawaida ameambia shirika la habari la ABC
Grandstand kwamba hajashangazwa na kitendo hicho cha Gayle.
Klabu ya Melbourne Renegades imesema matamshi hayo
yalikuwa hayafai kabisa na yalikuwa ya “kuvunja heshima”.
Maafisa wa klabu hiyo wameomba radhi kwa McLaughlin
na umma pia.
Pesa kutoka kwa faini aliyotozwa mchezaji huyo
zitakjabidhiwa wakfu wa McGrath unaosaidia watu wanaotatizwa na saratani ya
matiti.
0 comments:
Post a Comment