Image
Image

POLISI Njombe imeagizwa kusimamia fedha za maendeleo ya elimu kikamilifu.


POLISI Mkoa wa Njombe imeagizwa kuwa sehemu ya usimamizi wa fedha zilizo tolewa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya elimu Mkoa wa Njombe ili kuhakikisha pesa hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ya kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari kama alivyo agiza Mh Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi katika sherehe zilizoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe kusherekea mwaka mpya na kuwapongeza askari waliotimiza vyema majukumu yako ya kazi.
Aidha Dr Nchimbi ameonesha imani kuwa polisi wanaweza kulinda matumizi ya pesa hizo baada ya jeshi hilo kuonesha uwezo mkubwa wakusimamia usalama wa raia na malizao kipindi chote cha uchaguzi na kuwafanya wananjombe kuendesha shughuli zao kwa amani na utulivu hivyo kudhibitisha dhana ya uwepo wa maisha baada ya uchaguzi.
Dkt Nchimbi amesema kwa kuwa Jeshi la Polisi ni Sikio na Jicho la serikali hivyo alinabudi kujua ni kiasi gani cha pesa kilicho ingia Mkoa wa Njombe na kuhakikisha usalama wa pesa hizo na usalama wa walengwa wa pesa hizo ili kuepusha matumizi yasio sahihii, na ametoa onyo kali kwa walimu watakao ficha taharifa za pesa hizo.
“Pesa zilizoinginzwa Mkoa wa Njombe na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya elimu ni Nyingi, na zitakuwa zikiingizwa kila mwezi, hivyo tusipo zisimamia vizuri pesa hizi madhara yake yatakuwa ni makubwa, hivyo naliagiza Jeshi la Polisi Njombe, kupita pita na kutafuta taarifa sahii za mwenendo wa matumizi wa pesa hizi maana ninyi ndio Jicho na Sikio la Serilika, ili kama kunamwenendo mbaya wa matumizi tuchukue hatua kali kwa wahusika”, aliongeza Dr Nchimbi.
Aidha Dr Nchimbi ameonesha imani kuwa polisi wanaweza kulinda matumizi ya pesa hizo baada ya jeshi hilo kuonesha uwezo mkubwa wakusimamia usalama wa raia na malizao kipindi chote cha uchaguzi na kuwafanya wananjombe kuendesha shughuli zao kwa amani na utulivu hivyo kudhibitisha dhana ya uwepo wa maisha baada ya uchaguzi.
Nae Imamu wa msikiti Njombe Shehe UPETE katika kumtanguliza Mungu kwenye sherehiyo, amewaombea Askari wote wa mkoa huo ili mwenyezi Mungu awazidishie hekma na kuwapa afya njema ili wapate kuwatumikia vyema wakazi wa Njombe, Viongozi wa Juu serikalini na wananchi wote wa Tanzania kwa Ujuma.
Akimshukuru Mkuu wa koa kwa uzalendo aliouonesha kwa jeshi la Polisi Njombe, Kahimu Mkuu wa Polisi Njombe SSP JOHN TEMU ameahidi kufanyia kazi maagizo hayo na pia amewataka askari wote wa Jeshi la Polisi mkoani humu kufanya kazi kwa weledi ili kudumisha amani na upendo kwa wakazi wa Mkoa huo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment