Uongozi mzima wa Tambarare Halisi unawatakieni Hery
ya Mwaka mpya 2016,na kutoa shukrani za dhati kwa kutuamini na kuwa wenye
kusoma taarifa zetu kila zinapo tufikia hivyo mmezidi kutupa moyo wa kuendelea
kuwapasha habari kila muda zitufikiapo.
Mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka ambao kila mmoja aliuona
ni mwepesi na wengine kuona mgumu kwa kutofikisha lengo,nivyema sasa kwa mwaka
2016 kujipanga upya ilikuweza kukamilisha lengo.
Vilevile tunapenda kumpongeza Rais wa awamu ya Tano
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa na
kuanza kasi aliyoiahidi ya hapa kazi tu kwa kutumbua majipu ndani ya serikali
na taasisi mbalimbali kwa ukwepaji kodi na matumizi makubwa ya fedha yanayoligharimu
taifa na kuboresha sekta za afya na huduma za afya kuanza kupatikana mara
moja
Tunapenda kuona kwamba kwa kasi ya
Rais Magufuli kwa mwaka 2016 inapewa nguvu kuanzia watendaji ndani ya serikali
na jamii kiujumla ili tupate Tanzania mpya na yenye muonekano mpya kwa wananchi
kuanzia hali ya chini.
Pia mgogoro wa kisiasa Zanzibar ambao
haujapata muafaka toka mwaka jana licha ya vikao vingi kufanyika vya ndani ya
serikali ya Zanzibari hadi hivi leo ni faraja yetu tukija kuona kwa mwaka huu
Kasi hii ya hapa kazi tu itatue maramoja kusudi tuwe wa moja na tujenge nchi
kwa pamoja.
Mwaka jana 2015 Mwezi wa kumi na mbili
licha ya kuwa viongozi wote wa serikali ya Zanzibar wanao vutana kwa kila mmoja
alionana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
nakumueleza kila hatua inavyoendelea kwenye vikao vyao vya ndani ili
kukubaliana na kumaliza mgogoro huo lakini bado nadhani haitoshi kwa mwaka huu
ni vema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ukaona
ninamna gani hili suala linamalizika na kubaki historia kwani naamini hakuna
kinachoshindikana pakiwa na mazungumzo yenye mrengo wa amani na tija ya
kujenaga taifa.
Kila la Kheri Tumpe Nguvu Rais afanye
anayoyakusudia nasi tunaahidi tutakuwa naye bega kwa bega.
0 comments:
Post a Comment