Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli amemhakikishia Waziri Mkuu wa Israel kuwa Serikali ya awamu ya
tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kushirikiana na kuimarisha
zaidi mahusiano kati ya Tanzania na Israel katika nyanja mbalimbali ili kuleta
manufaa kwa pande zote.
Rais Magufuli amesema hayo alipokutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Nairobi - Kenya
Mheshimiwa Yahel Vilan, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Aidha Rais Magufuli ameahidi kuwa Tanzania itahakikisha
inaanzisha ubalozi wake nchini Israel haraka iwezekanavyo.
Kwa upande wake Balozi wa Israel hapa nchini Yahel
Vilan pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri na kubwa anayoifanywa na
uongozi wake katika kipindi kifupi cha miezi miwili tangu aingie madarakani amemuhakikishia
kuwa Israel itaendelea kushirikiana na Tanzania na ipo tayari kuimarisha zaidi
mahusiano yake.
Balozi Vilan ametaja baadhi ya maeneo ya ushirikiano
kuwa ni pamoja Kilimo,Maji,Ufugaji wa Nyuki na Sayansi na Teknolojia huku
akibainisha kuwa Israel imewaalika jumuia ya wafanya biashara wa Tanzania
kushiriki katika kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Israel litakalo
fanyika mjini Tel Aviv nchini Israel Mwezi Septemba Mwaka huu.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi Yahel Vilan wa Israel hapa nchini Ikulu Jijini Dar es salaam Januari 19, 2016 baada ya kufanya naye mazungumzo
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Balozi Yahel Vilan wa Israel hapa nchini kabla ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam Januari 19, 2016
0 comments:
Post a Comment