Mwanamuziki wa Bongo Flava nchini Tanzania TID
ambaye amekuwa anafanya muziki huo kwa muda mrefu amefunguka juu ya kumsainisha
kwenye kampuni yake ya Radar Entertaiment Mwanamuziki wa Muda mrefu KR.MULLER
jibabaa ili kufanya kazi baada ya kutoka kwenye kundi la TKM wanaume halisi.
TID amesema kuwa licha ya KR.MULLER kuwa na jina
kubwa ilimlazimu kusainisha kwenye kampuni yake baada ya kugundua kwamba jina
la MULLER bado ni nembo ya Muziki wa Bongo flava Nchini Tanzania.
Amesema wakati wa kampeni za kumnadi Mh.Kassim
Majaliwa jimboni mwake ambambo yeye TID pamoja na wasanii wengine akiwamo KR.MULLAR
wakati wakiwa kwenye gari wakielekea lindi kila waliposimama na hata kutembea
ndani ya gari sauti za wananchi hazikusita kuita jina la KR.MULLER kitendo
kilicho mfanya atafsiri kuwa licha ya wingi wa wasanii ndani ya gari lakini
bado MULLER alikuwa kioo chao/
Amesema kwa sasa tayari kila kitu kipo sawa kabisa
hivyo kuachia ngoma kwa MULLER ni muda wowote hivyo jina la msanii huyo
litarudi sehemu yake.
Kwa sasa baada ya kampuni yake ya Radar Entertaiment
kuanza na Bill Nas ambaye yupo chini ya Radar Entertainment ambaye
amekuwa akifanya vizuri na wimbo wake wa Lg Ndogo aliomshirikisha Naazizi
kutoka Kenya na TID mwenyewe.
0 comments:
Post a Comment