Wagombea wa uraisi 20 kati ya 20 nchini Jamhuri ya
Afrika ya Kati wametoa wito wa kura zilizopigwa kufutwa kwa madai ya kuwepo kwa
ulaghai.
Matarajio yalikuwa baada ya uchaguzi huo wa Jumatano
wiki iliyopita kwamba hali ya amani ingeweza kurudi nchini humo ambako maelfu
wamefariki dunia katika vita vya kidini.
Kura zaidi ya robo zimehesabiwa na Waziri mkuu wa
zamani Faustin Archange Touadera, ndiye anayeongoza kwa sasa.
Msemaji wa kundi la wagombea hao 20, Théodore Kapou,
amewaambia waandishi wa habari kuwa hawaridhishwi na jinsi uchaguzi huo
uliendeshwa. "Sisi, wagombea kwa uchaguzi wa urais, watia sahihi wa tamko
hili, tunakataa ushirika wa uchaguzi batili kama huu.Tunatangaza kuwa mchakato
wa uchaguzi si wa kuaminika. Ni lazima usimamishwe ili ushirikiano uwepo na
utekelezwaji uendele."
0 comments:
Post a Comment