Wananchi
2,857 walioptwa na mafuriko yaliyosababisha yumba zaidi ya 379 kubomoka na
nyingine 997 kuingia maji katika kata ya magomeni wilaya ya kilosa mkoani
Morogoro wameanza kupatiwa misaada ya chakula ingawa inahitajika misaada ya
haraka ya dawa za binadamu, vyandarua pamoja na mahema ili kuwakinga na maradhi
yanayoweza kujitokeza.
Wakizungumza
wakati wa kupokea misaada hiyo waathirika wa mafuriko hayo wamewashukuru
kampuni ya Alsaid pamoja na wabunge akiwemo mbunge wa viti maalumu mkoa wa
Morogoro Devota Minja kwa jitihada zao walizo zionyesha toka kutokea kwa
mafuriko hayo huku wakiomba serikali kuwasaidia kwa mambo mengine kama
Mahema,vyandarua, pamoja na dawa kwa kujikinga na magonjwa ya milipuko.
Kwaupande
wake mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya ALSAID Mbaraka Alsaed amesema kampuni
yake itaendele kuwasaidia wahanga hao huku akiziomba taasisi mbalimbali na
mashirika kuwasaidia wahanga hao ilinao waweze kuishi hasa katika kipindi hiki
kigumu kwao.
Nao wabunge
akiwemo mbunge wa jimbo la kilosa Mbaraka Bawaziri ameshukuru misaada
mbalimbali inayo endelea kutolewa na wahisani huku mbunge viti maalumu mkoa wa
morogoro devota minja akisema ipo haja ya serikali kuangalia swala la ujenzi wa
tuta la mto mkondoa ili lisiendelee kesababisha hasara kwa watanzania na
serikali.
0 comments:
Post a Comment