Wakazi zaidi ya 400 hawana mahala pa kuishi baada ya
nyumba 70 kusombwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha katika
eneo la kijiji cha Mpunguzi kilichopo Manispaa ya Dodoma.
Baadhi ya wakazi waliokumbwa na mafuriko hayo
wamesema hali hiyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kwa kile wanachodai ni
udogo wa daraja lililopo barabara kuu ya Dodoma Iringa linalokatisha eneo hilo
kushindwa kuhimili wingi wa maji na kujenga mkondo ambao umesambaa na kuyafikia
makazi yao na kuzua balaa hilo ..
Kufuatia janga hilo kaimu afisa mtendaji wa kijiji
cha Mpunguzi Dionuis Samo amesema mafuriko hayo ambayo ni mara ya pili kutokea
kwa kipindi cha wiki mbili ameiomba serikali kupitia wakala wa barabara nchini
TANROADS kulitafutia ufumbuzi wa haraka eneo hilo ili lisiendelee kuleta
madhara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Dodoma…
Mvua hizo pia zimeripotiwa kusababisha maafa katika
kata za Kigwe wilayani Bahi, Nzuguni Manispaa ya Dodoma na kijiji cha Matumbulu
ambapo kwa mujibu wa viongozi wa serikali katika maeneo hayo wanadai zaidi ya
watu 400 wameathirika .
0 comments:
Post a Comment