Gavana wa jimbo la Florida, Rick Scott ametangaza
hali ya dharura katika Kaunti nne kutokana na virusi vya Zika.
Kesi tisa za ugonjwa huo zimegunduliwa jimboni
Florida.
Maafisa wa afya wanaamini kuwa maambukizi hayo
yametokea baada ya watu kusafiri kwenye nchi zilizoathirika.
Virusi vya Zika vinavyosababisha dosari kwenye
ubongo kwa watoto,vimekuwa hoja inayozungumzwa sana ulimwenguni.
Virusi hivi husambazwa na mbu, lakini wachunguzi wa
maswala ya afya wanasema huenda virusi hivi vinasambazwa kwa njia ya
kujamiiana.
Maafisa wa masuala ya afya nchini Marekani wamesema
mtu mmoja jimboni Texas aliathirika na virusi vya Zika kwa njia ya kujamiiana,
hlo ni tukio la kwanza la ugonjwa huo kutokea nchini Marekani.
0 comments:
Post a Comment