Jaji Mkuu wa Kenya Dokta Willy Mutunga ameishauri
Serikali ya Tanzania kuharakisha mchakato wa Katiba Mpya iliyopendekezwa
ili itoe fursa kwa mahakama nchini kufanya kazi zake kwa uwazi na weledi pamoja
na kuwashirikisha wananchi hasa katika uteuzi wa majaji wakuu.
Amesema, ili hilo litekelezwe kwa ufanisi Katiba
pekee ndiyo jibu la kuleta maendeleo katika Nyanja zote kwani itaweza
kuzingatia masilahi ya Watanzania na nchi kwa ujumla.
Jaji Mutunga ameyasema hayo wakati wa mazungumzo
maalumu na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na mwenyeji
wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Chande Othman Chande katika Mahakama Kuu ya
Tanzania. Jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo yao yenye lengo la kubadilishana
uzoefu wa kimahakama, ni pamoja na mabadiliko ya Katiba ya Kenya, Uhusiano wa
Mahakama na Wananchi ambapo Jaji Mutunga amesema, uteuzi wa Majaji wakuu nchini
mwake sasa unashirikisha wananchi tofauti na awali ambapo Katiba ilikuwa
ikikiuka.
Kuhusu Kurejewa tena kwa mchakato wa upatikanaji wa
Katiba Mpya, Dk Mutunga amesema itatoa fursa kwa mahakama nchini kufanya kazi
zake kwa uwazi na weledi pamoja na kuwashirikisha wananchi hasa katika uteuzi
wa majaji wakuu.
Pamoja na Kila nchi kuwa na utaratibu wake katika
mihimili mikuu ya Serikali Jaji Chande Othman Chande amekiri kuongezwa uwazi
zaidi kwa wananchi huku akianisha baadhi ya hatua za kuteua majaji wakuu
nchini.
Ziara ya Jaji Mkuu huyo wa Kenya imekuja ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo yanafikiwa kilele Alhamisi hii,
huku mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Dk Magufuli.
0 comments:
Post a Comment