Image
Image

Iran iko tayari kwa ajili ya uchaguzi wa Bunge na Baraza la Wataalamu


Muda wa kampeni za uchaguzi wa Bunge na Baraza la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Iran umemalizika mapema leo saa mbili asubuhi tarehe 25 Februari na wananchi wa Iran kesho Ijumaa wataelekea kwenye masanduku ya kupigia kuwachagua wawakilishi wao katika zoezi litakaloanza asubuhi na kuendelea kwa masaa kumi.

Katika uchaguzi huo Wairan watawachagua wabunge 290 na wawakilishi 88 wa Baraza la Wataalamu.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran, Abdul Ridha Rahmani Fazli ametangaza kwamba, maafisa wa kusimamia zoezi hilo wamejitayarisha kikamilifu kwa ajili ya uchaguzi huo. Amesema kuwa uchaguzi ni awamu muhimu ya kuimarisha tena uwezo na nguvu ya wananchi na azma ya kuijenga na kuistawisha Iran na kuongeza kuwa: Masanduku laki moja na elfu 20 na maafisa milioni moja wako tayari kwa ajili ya kusimamia zoezi hilo litakalofanyika kesho Ijumaa.
Waziri Rahmani Fazli ameshiria uelewa na umakini wa taifa la Iran katika kukabiliana na njama za maadui wa kigeni ikiwemo Uingereza na ametoa wito wa wananchi kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo kwa ajili ya maslahi ya kitaifa. Amesema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa na tasisi mbalimbali, inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia sabini ya wananchi waliotimiza masharti watashiriki katika zoezi hilo la kupiga kura.
Karibu Wairani milioni 55 wametimiza masharti ya kupiga kura katika chaguzi hizo mbili.
Waandishi habari 473 kutoka nchi 29 duniani wapo hapa nchini kwa ajili ya kuripoti matukio ya uchaguzi wa kesho.
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu pia amewataka wananchi wote waliotimzia masharti kushiriki kwa wingi na kwa nishati katika zoezi hilo la kidemokrasia ili kuzidisha nguvu ya taifa na rasilimali ya kijamii ya Iran kwa kuonesha umoja na maadili ya Kiislamu. Amesema mahudhurio makubwa ya wananchi katika uchaguzi wa kesho yana umuhimu mkubwa na kuongeza kuwa, taifa la Iran litashinda mtihani huo kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizotangulia.
Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran, Ayatullah Hashemi Rafsanjani pia ametoa wito wa kushiriki kwa wingi wananchi katika uchaguzi wa kesho na kusema kuwa, mahudhurio makubwa ya wananchi yatabatilisha njama za maadui wa Iran ya Kiislamu.
Viongozi waandamizi wa kidini pia wamewahimiza wananchi wa Iran kushiriki ipasavyo katika uchaguzi wa kesho na kuonesha hamasa nyingine.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Iran, Dakta Ali Larijani amesema kuwa kushiriki kwa wingi wananchi katika zoezi hilo kutapandisha juu hadhi ya taifa la Iran duniani kote. Ameongeza kuwa hali ya sasa ya eneo la Mashariki ya Kati na ulimwenguni imezidisha umuhimu wa uchaguzi wa kesho hapa nchini.
Wakati huo huo makundi ya waliowachache hapa nchini kama Mayahudi na Wazartoshti yametangaza kuwa yamejitayarisha ipasavyo kwa ajili ya chaguzi za Bunge na Baraza la Wataalamu.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa kila moja kati ya makundi ya Mahahudi, Wakrito na Wazartoshti wana mwakilishi mmoja katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge).
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment