Kaya zaidi ya laki moja na nusu katika wilaya za
Bukoba, Missenyi na Ngara, mkoani
Kagera zinatarajia kunufaika na mradi wa
unyunyuziaji wa dawa ya kuzuia mbu majumbani wanaoambukiza ugonjwa wa Malaria.
Takwimu zinaonesha kuwa maambukizi ya ugonjwa huo
yamepungua kwa asilimia 41 toka mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 8.5.
Hayo yamebainika katika uzinduzi wa mradi wa
unyunyuziaji dawa majumbani unaofadhiliwa na serikali ya
Marekani ambao umezinduliwa kimkoa katika kata ya Kabale
wilayani Bukoba mkoani Kagera.
Akizindua mradi huo mkuu wa mkoa wa Kagera John
Mongella, amewataka viongozi wote mkoani humo kuanzia ngazi za vijiji
kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja ili kila kaya iliyolengwa katika mradi
huo iweze kupata huduma , huku akiwataka watoa huduma kufanya kazi hiyo
kwa uadilifu ili jamii iweze kufaidika ipasavyo.
Kwaupande wake msimamizi wa mradi huo nchini
Dr.Nduka Iwuchukwu (EUCHU), amewataka wananchi kutoa ushirikiano mara tu
watakapofikiwa kupatiwa huduma hiyo ya unyunyuziaji wa dawa ya mbu majumbani.
Aidha, licha ya mradi huo kupokelewa vizuri na
wananchi mkoani humo, mganga mkuu mkoani Kagera Dr Thomasi Rutachunzibwa
amesema zoezi hilo litakuwa chachu ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa
malaria kwa asilimia kumbwa.
Pindi utakapo anza kutekelezwa mradi huo
wa unyunyuziaji wa dawa ya ukoko unatarajia kutoa zaidi ya
ajira zipatazo elfu moja miambili tisini na mbili, kwa lengo lakufanikisha
zoezi hilo litakalofanyika kwa muda wa wiki tatu.
0 comments:
Post a Comment