Waendesha mashtaka nchini Brazil wamependekeza
kwamba nyota wa timu ya Barcelona Neymar ashtakiwe na mashtaka matatu ya
ufisadi kuhusu kesi ya kodi wakati wa uhamisho wake hadi Barcelona.
Inadaiwa kwamba kampuni zilibuniwa ili kutumika kwa
niaba yake ili mchezaji huyo alipe kodi ya kiwango cha chini.
Maafisa nchini Brazil wanasema kuwa madai hayo dhidi
ya mshambuliaji huyo wa Barcelona yanasimamia kipindi cha miaka saba kuanzia
2006.Madai hayo ni tofauti na yale ya kesi iliosikizwa siku ya Jumanne nchini
Uhispania.
Neymar alihudhuria kesi yake ya madai ya ufisadi
kuhusu uhamisho wake.Amekana kufanya makosa yoyote.
Waendesha mashtaka wa serikali ambao wanapendekeza
kushtakiwa kwake wanadai kwamba kampuni zilibuniwa na fedha ambazo
zingelipishwa kodi katika kiwango cha mtu binafsi zilitumwa katika kampuni hizo
ili kupunguza ada hiyo.
Ni mapema mno.
Madai hayo ya viongozi wa mashtaka yatakwenda kwa
jaji ambaye ataamua iwapo kuna kesi ya kujibu au la.kwa sasa Neymar sio
mshtakiwa.
0 comments:
Post a Comment