Jamie Vardy aliwafungia Leicester mabao mawili na
kuwawezesha kulaza Liverpool na kuelendelea kukwamilia kileleni Ligi ya Premia.
Klabu hiyo imo alama tatu kileleni mbele ya
Manchester City.
Mshambuliaji huyo Mwingereza alifunga bao la kwanza
kwa kombora la hatua 25 kutoka kwa goli baada ya kupokea pasi kutoka kwa Riyad
Mahrez dakika ya 60.
Na alikamilisha ushindi wao baada ya kufunga mpira
wa Shinji Okazaki uliokuwa umepinduliwa dakika ya 71.
Kwingineko, Arsenal walipoteza alama baada ya kutoka
sare tasa na Southampton nyumbani, jambo lililowafanya kupitwa na Tottenham.
Manchester United hata hivyo walitamba kwa ushindi
wa 3-0 dhidi ya Stoke City uwanjani Old Trafford, mabao yao yakifungwa na Jesse
Lingard (14’), Antony Martial (23’) na Wayne Rooney (53’).
Leo jioni, Chelsea watakuwa ugenini Watford, nao
Everton wawe nyumbani Goodison Park dhidi ya Newcastle. ,
Arsenal 0 -0 Southampton
Leicester 2-0 Liverpool
Norwich 0-3 Tottenham
Sunderland 0-1 Man City
West Ham 2-0 Aston Villa
Crystal Palace 1-2 Bournemouth
Man Utd 3-0 Stoke
West Brom 1-1 Swansea
0 comments:
Post a Comment