Maafisa wa afya nchini Marekani wanachunguza taarifa
nyingine 14 za uwezekano wa kuenezwa kwa virusi vya Zika kwa njia ya
ngono.
Visa hivyo vinahusisha wanawake kadhaa wawajawazito,
kilieleza kituo cha CDC.
Kituo cha Marekani cha udhibiti wa magonjwa (CDC)
kimefichua hayo wakati kikizindua muongozo mpya juu ya maambukizi ya virusi hivyo
kwa njia ya ngono .
Muongozo huo umetolewa kufuatia kuthibitishwa kwa
kisa cha kwanza cha Zika kwa mtu ambae hakusafiri nchini Marekani.
Kisa hicho kilikuwa na uhusiano na tendo la
kujamiiana na mpenzi alieambukia virusi vya Zika.
Kituo cha CDC kinawashauri wanaume wote ambao
wamesafiri kwenye maeneo yenye virusi vya Zika kutumia mipira ya kondomu ama
kuacha kufanya tendo la ngono kwa kipindi cha ujauzito.
Hakuna ushahidi bado kwamba wanawake wanaweza
kueneza virusi vya Zika kwa wapenzi wao, lakini utafiti zaidi unahitajika
kuelewa suala hili, kilieleza kituo hicho cha afya ya mwili.
Njia kuu ya maambukizi ya Zika kwa sasa bado ni
kuumwa na mbu.
Wataalam wanasema wanawake wajawazito wanapaswa
kujaribu kuepuka kuumwa na wadudu.
Jumanne, Margaret Chan, mkuu wa Shirika la Afya
Duniani, alisema kuwa dunia inakabiliwa na "safari ndefu "ya
kutokomeza Zika.
Akizungumza nchini Brazil, ambako visa vingi
vimeripotiwa, alisema kuwa "virusi vya Zika ni vigumu, na itahitaji ujuzi
wa hali ya juu " kuviangamiza.
0 comments:
Post a Comment