Shirikisho la Mpira wa Kikapu ( NBA) litazindua
rasmi msimu wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana kwenye kituo cha
vijana cha Michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dar es Salaam mnamo tarehe
27 Februari mwaka huu.
Sherehe hii ya ufunguzi wa mashindano hayo
itahudhuriwa na Mchezaji Nyota wa mchezo huo na Mwandamizi wa shirikisho la
Mpira wa kikapu Ulimwenguni Allison Feaster utakuwa ni uzinduzi rasmi wa ligi
ya Mpira wa Kikapu kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 12 na 14.
Ligi hii itajumuisha shule zipatazo thelathini (30)
kutoka maeneo ya karibu na kila shule ikiwakilisha moja wapo ya timu 30
zinazoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani.
Ligi ya mpira wa kikapu ya vijana (Jr. NBA League)
ni ligi ya NBA ya dunia inayoshirikisha mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana,
wavulana kwa wasichana na inafundisha stadi za msingi za mchezo wa mpira wa
kikapu pamoja na maadili muhimu ya mpira wa kikapu kwa wachezaji wanaoanza,
Lengo likiwa ni kusaidia kukuza na kuboresha uzoefu wa Wachezaji, Makocha na
Wazazi.
0 comments:
Post a Comment