Mgombea wa urais wa chama cha Republican Donald
Trump ameshinda katika jimbo la Nevada nchini Marekani, na hivyobasi kuimarisha
uongozi wake katika mchujo wa kuwania tiketi ya chama hicho.
Tajiri huyo sasa ameshinda mara tatu ,kufuatia
ushindi wake katika jimbo la New Hampshire na Carolina kusini.
Seneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao wamekuwa
wakishambuliana wiki hii wanapigania nafasi ya pili.
Maafisa wa chama hicho wamesema wamekuwa
wakichunguza ripoti za watu kupiga kura mara mbili huku eneo moja likidaiwa
kuwa na vifaa vichache vya kupigia kura.
Baadhi ya watu waliojitolea pia walidaiwa kuvaa nguo
zenye picha za bwana Trump,lakini maafisa wamesema kuwa hatua hiyo sio kinyume
na sheria.
0 comments:
Post a Comment