Image
Image

Mpesya asisitiza mahusiano kati ya Tanzania na Msumbiji.



Mkuu wa Wilaya Songea,BENSON MPESYA amewatembelea wananchi  wanaosihi mpakani mwa Tanzania na Msumbiji  na kusisitiza  kuendelezwa uhusiano mwema kati ya wananchi wa Mji wa  Congress nchini Msumbiji  na Mkenda nchini Tanzania.
Akiwa Mjini  Congress  nchini Msumbiji,Mkuu wa Wilaya ya Songea amesisitza uhusiano mzuri  wa watumishi wa Serikali wa Tanzania na Msumbiji ili  pamoja na  wananchi wa pande zote mbili wajione kuwa ni ndugu.
Ziara hiyo imekuja  siku chache baada ya kuripoti  matatizo yanayowakabili  wananchi  wanaoishi  mpakani  mwa Tanzania na  Msumbiji .
Naye Afisa Uhamiaji  wa  Mji wa Congress nchini  Msumbiji,ARCANJO DOMINGOS  ameeleza kuwa Mji wa  Congress ume pewa  jina hilo kutokana na mikutano ya ukombozi  iliyokuwa ikifanyika  mjini humo na kwamba kuna uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Msumbiji .
Kati ka ziara yake hiyo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji,MPESYA  ametembelea shule ya msingi Kivukoni iliyoharibiwa kwa ufa na kufanya watoto wasomee kwenye vibanda vilivyoezekwa kwa nyasi na pia ametembelea eneo yanakojengwa majengo mapya ya shule na kuahidi kupiga kambi siku mbili  huko akishirikana  na wananchi katika  ujenzi .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment