Image
Image

Mawakala wa TRA wafungia mgodi wa alimasi wa El HILALI Shinyanga.

Mamlaka ya Mapato Tanzania -TRA-Mkoani Shinyanga imeufunga mgodi wa alimasi wa El HILALI ulioko Mwadui Shinyanga kwa muda usiojulikana .
Uamuzi huo umetokana na  kosa la kushindwa kulipa deni la mapato ya Serikali Shilingi milioni miatatu sabini na nne na laki tisa na sabini huku wafanyakazi wa mgodi huo wakilalamik a kuathiriwa na kitendo hicho.
Akizungumza na  Radio One Stereo kuhusu sakata la kufunga mgodi huo wakala wa ukusanyaji mapato wa TRA LYASUKA IBRAHIM amedai TRA imelazimika kuufunga mgodi  huo hadi kiasi cha deni linalodaiwa litakapolipwa.
Naye Kaimu Meneja wa kitengo cha  uzalishaji katika mgodi huo,BADER SEIPH alipoulizwa kwa nini amekiuka amri ya kusitisha uzalishaji na kuruhusu magari kuendelea kusomba kifusi chenye madini ya alimasi alikataa na kudai hakuna kazi inazoendelea mahali hapo.
Lakini  Maa fisa wa TRA walipofuatilia walikuta magari sita yakiendelea kufanya kazi na kulazimika kuyakamata na kuyapeleka katika yadi ya TRA ili yopo mjini shinyanga kwa hatua ny ingine zaidi.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment