Chama cha wananchi CUF kimeendelea kusisitiza kutoshiriki
uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika machi 20 mwaka huu visiwani Zanzibar
na kusema hali ya usalama visiwani humo inaendelea kuwa mbaya kutokana na
kuibuka kwa kikundi cha watu wanaojiita Mazombi kinachovamia watu na kuwapiga
na sasa kimeanza kuvamia ofisi za CUF huku serikali ikilalamikiwa kukaa kimya
kuhusu wahalifu hao.
Katibu mkuu wa cuf na aliyekuwa mgombea urais visiwani
Zanzibar maalum Seif Sharif Hamada ameyasema hayo jijini Dar es Salaam baada ya
kuwa na mazungumzo ya saa moja unusu juu ya hali haki si ya kisiasa visiwani
Zanzibar na aliyekuwa mgombea wa urais wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA
Mh.Edward Lowassa na kusema hali ya vitisho imeendelea kujitokeza pia kwa
watumushi wa serikali ambao vitambulisho vyao vimechukuliwa na kutakakiwa
kusajiliwa namba hivyo ni ukiukwaji wa demokrasia.
Kadhalika Maalim Seif ameitaka serikali kuchua hatua haraka
kwa kikundi ambacho kimeibukia visiwan zanzibar ambachi kimekuwa kikiteka watu
na kuwapiga na sasa kimeanza kuvamia na kuharibu ofisi za CUF ambapo hivi
karibuni kikundi hichi kilivamia ofisi ya CUF huku msumbiji na kuiteketeza kwa
kuharibu samani zake zote.
Aliyekuwa mgombea urais kupitia umoja wa katiba ya wananchi
UKAWA Mh.Edward Lowassa yeye amesema suala za Zanzibar linahitaji kutatualiwa
kwa njia ya majadiliano na sio ubabe wa kutaka kulazimisha kurudiwa kwa
uchaguzi na kama vurugu zitatokea zanzibar basi pia zitasababisha matatizo na
madhara makubwa kwa tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment