Rais Dakta.John Pombe Magufuli amesema hataingilia
mgogoroo wa Zanzibar na kuwataka wenye malalamiko waende Mahakamani.
Akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam
amesema hakusudii kamwe kuingilia mzozo huo na kwamba ataendelea kukaa kimya na
anayetaka tafsiri aende mahakamani lakini atakayeleta vurugu vyombo vya usalama
vipo.
Pia akizungumza na wazee hao Rais DR. JOHN POMBE
MAGUFULI ameagiza jengo jipya la la ghorofa la utawala kwa ajili ya
mipango ya uzazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam
liwe wodi ya wazazi ili kupunguza msongamano wa wazazi katika wodi yao ya sasa.
Ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya wazee wa Dar es
salaam iliyoandaliwa kuadhimisha siku 100 za uongozi wake kufuatia ziara yake
ya hspitali ya Muhimbili hapo juzi aliposhuhudia hali mbaya ya msongano wa
wazazi katika wodi yao ya sasa.
Aidha katika hafla hiyo Rais MAGUFULI alisema
serikali yake imedhamiria kuibadili Tanzania na kwamba ingawa katika mabadiliko
kuna changamoto zake lakini watakaoguswa ni wachache na siyo wananchi wa
kawaida.
Amesema Tanzania siyo nchi maskini lakini kuna watu
wachache ambao wanatafuna nchi na ndiyo maana ameamua kutumbua majipu na kutala
viongozi wake wawajibike na watakaojaribu kukwamisha nia ya serikali
watatimuliwa.
Mapema Makamu wa Rais Mama SAMIA SULUHU HASSAN na
Waziri Mkuu Mheshimiwa KASSIM MAJALIWA walisema wale wanaosema kasi iliyoanzwa
na serikali ya awamu ya tano ilikuwa nguvu ya soda wataisoma namba.
Walisema wataendelea kuwahudumia wananchi na
Watanzania wasiwe na mashaka kwani wamejipanga vizuri na wanatambua wanayotaka
na katika kuwajibika watapita huko huko waliko kuwatimiza mahitaji yao na
kutaka Watanzania wawaombee huku rais mwenyewe pia akiahidi Tanzania itaenda
mbele kwa maendeleo ya Watanzania wote.
0 comments:
Post a Comment