Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameahidi kuwa uchaguzi mkuu
utakaofanyika kesho utakuwa wa amani na mtu yeyote atakayejaribu kuzusha vurugu
ataadhibiwa vikali.
Rais Museveni amesisitiza haja ya kudumisha amani na utulivu
wa nchi na kusema hii itasaidia kuhimiza maendeleo na kudumisha mafanikio ambayo
yamepatikana hadi leo.
Mapambano yalitokea juzi kati ya polisi wa Uganda na wafuasi
wa mgombea urais wa chama cha upinzani kwenye sehemu ya katikati ya mji wa
Kampala, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine wengi kujeruhiwa.
0 comments:
Post a Comment