Mwalimu mmoja wa shule ya Madrasa,ametambuliwa kuwa mshukiwa
aliyetekeleza shambulio la bomu ambalo lilisababisha shimo kubwa katika tanki
ya mafuta ya ndege moja ya abiria nchini Somalia, iliyokuwa ikielekea nchini
Djibouti, tarehe mbili Februari mwaka huu.
Abdullahi Abdisalam Borleh, alirushwa na mlipuko uliotokea
katika ndege hiyo aina ya Airbus 321, wakati bomu hilo lilipolipuka muda mfupi
baada ya ndege hiyo kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mogadishu.
Maafisa wa idara ya ujasusi wanaamini kuwa Borley, ambaye
anatoka eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland, alibeba bomu hiyo
kimakusudi.
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab, lilidai
kuhusika na mlipuko huo, lakini halijatoa majina ya waliohusika moja kwa moja.
Hamna aliyeuawa wakati wa mlipuko huo, ambao ulitokea dakika
kumi na tano baada ya ndege hiyo kupaa.
Ndege hiyo ililazimika kurejea na kutua kwa dharura katika
uwanja wa ndege wa Mogadishu nchini Somalia.
0 comments:
Post a Comment