Tanzania imepokea wakimbizi laki 1.3 kutoka Burundi kuanzia
mwezi Aprili mwaka jana hadi mwezi huu. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya
Tanzania Bw Isaac Ntantanga amesema ujio wa wakimbizi hao ulianza mwaka jana
wakati mgogoro ulipozuka.
Kwa sasa wizara ya mambo ya ndani ya Tanzania kwa
kushirikiana na Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na
wadau wengine wako mstari wa mbele kuendelea kuwapatia wakimbizi hao msaada
ikiwa ni pamoja na chakula, maji na ulinzi.
Habari pia zinasema kikosi cha nchi za Afrika Mashariki
kimewekwa tayari kuingia nchini Burundi chini ya mwavuli wa kikosi cha Umoja wa
Afrika kama serikali ya Burundi itaruhusu kikosi hicho kuingia nchini Burundi
0 comments:
Post a Comment