Mwalimu wa shule ya msingi Mwagimaji iliyopo kata ya
Nyanguku Mjini Geita Hamis Mumwi anayedaiwa kumpa mimba mwanafunzi kisha kumuoa
ameendelea kuishi katika darasa moja lililopo katika shule hiyo na familia yake
takribani miaka 10 licha ya kufukuzwa kwa kosa hilo.
Mwalimu huyo imedaiwa alifukuzwa mwaka 2002 na
amekuwa akiishi katika darasa hali ambayo imechangia wanafunzi wa shule hiyo
kuwa na vyumba vichache na kusababisha darasa moja kukaa wanafunzi wa madarasa
tofauti.
Shule ya Mwagimagi ina jumla ya wanafunzi 418 na
madarasa sita lakini kwa sasa yamebaki matano kutokana na mwalimu kuishi
darasani.
Mwalimu Mumwi anaishi hapo baada ya nyumba alokuwa
anaishi kubomoka na kuhamia darasani na hatoki hadi hapo Halmashauri
itakapomlipa stahiki zake.
Mumwi amekataa kuwa hakuoa mwanafunzi bali
alimaliza darasa la saba na hakuendelea na masomo ndipo alimpa mimba na
kumuona.
Amedai alifukuzwa kazi mwaka 2002 baada ya kushindwa
kesi kwenye mahakama ya mwanzo lakini baadae alikata rufaa na kushinda kesi
kwenye mahakama ya wilaya na mwajiri kutakiwa kumrudisha kazini ambapo alirudi
hadi mwaka 2005 alipofukuzwa tena kwa mara ya pili.
Diwani wa Kata ya Nyanguku Elias Ngole aliliibua
suala hili katika kikao cha Baraza la Madiwani mbapo Mwenyekiti wa Halmashauri
alitaka hatua zaidi zichukuliwe.
Diwani Kata ya Nyanguku Elia Ngole amesema
Imeonekana kuwa mwalimu Mumwi alipofukuzwa taratibu zote za kisheria
zilifanyika ikiwemo kumsafirisha na familia yake kwenda kwao ukerewe lakini
alirudi shuleni hapo.
Afisa utumishi wa halmashauri ya mji Laurence
Mhelela amebainisha kuwa Mumwi hadai stahiki zozote kwa kuwa alifukuzwa kazi
toka mwaka 2005 lakini kwa sasa wanachukua hatua za kulimaliza suala hilo.
0 comments:
Post a Comment