Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa nchini
Dk.Hussen Mwinyi amesema jeshi hilo limeanza kuchukua hatua stahiki za kijeshi
dhidi ya askari ambao wamekua wakienda kinyume na
sheria,mila na desturi za jeshi katika kipindi chote tangu jeshi lianzishwe
mwaka 1964.
Waziri ameyasema hayo dodoma wakati akijibu swali la
mbunge viti maalum Mh.Maryam Msabaha aliyetaka ufafanuzi kuhusu
hatua za kinidhamu zinazochukuliwa kwa askari wanaokiuka haki za binadamu na
kwenda kinyume na sheria katika utendaji wao wa kazi hasa kutumia nguvu nyingi
kwa wananchi.
Dk .Mwinyi amesema jeshi limekua likichukua
hatua stahiki za kijeshi dhidi ya wakosaji kwa mujibu wa taratibu zake na
wengine kupelekwa mahakamani za kiraia kulingana na aina ya kosa alilotenda muhusika
na kwa wale waliokutwa na hatia walipewa adhabu stahiki kulingana na uzito w a
makosa waliotenda ikiwa ni pamoja na vifungo vilivyoambatana na kufukuzwa
utumishi jeshini
Ameongeza kwa kusema kuwa ni
vigumu kubainisha idadi ya askari hao tangu
jeshi lianzishwe ambapo kimsingi jeshi
limekuwa likichukua hatua stahiki za kijeshi dhidi ya wakosaji kwa
mujibu wa taratibu zake na wengine kupelekwa
katika mahakama za kiria kulingana n aina ya kosa
alilotenda mhusika
0 comments:
Post a Comment