Wanajeshi wa Uganda wakishirikiana na maafisa wa polisi
wamevamia na kuzingira afisi za chama cha upinzani za Forum for Democratic
Change (FDC).
Kiongozi wa chama hicho, Dkt Kizza Besigye, ambaye amekuwa
akiwania urais amekuwemo ndani ya afisi hizo na mwandishi wa BBC Patience
Atuhaire anasema polisi wameondoka naye akiwa kwenye gari lao.
Kituo cha televisheni cha NBS kimeripoti kuwa Besigye na
rais wa FDC Mugisha Muntu wamekamatwa katika makao makuu hayo eneo la
Najjanankumbi, na wafuasi wa chama hicho wakatawanywa kwa kutumia mabomu ya
kutoa machozi.
Mgombea mwingine wa urais Amama Mbabazi amepakia video
kwenye Twitter inayoonesha maafisa wa usalama nje ya nyumba yake. Anasema
polisi wameanza kuwakamata watu nje ya nyumba yake.
Viongozi wa chama cha FDC walikuwa wakijiandaa kuhutubia
wanahabari kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika jana.
Maafisa wa usalama wanashika doria kwa wingi maeneo
yanayozunguka makao makuu hayo ya chama cha FDC, mwandishi wa BBC Catherine
Byaruhanga anasema.
Milio inasikika ingawa haijabainika iwapo ni ya risasi
halisi, risasi za mipira au mabomu ya kutoa machozi.
Hii ni mara ya tatu kwa Dkt Besigye kukamatwa wiki
hii. Alikamatwa
jana jioni katika kitongoji cha Naguru, mjini Kampala katika nyumba ambayo
upinzani ulidai wizi wa kura ulikuwa ukifanyika.
Jumatatu, alizuiliwa kwa muda wakati akifanya kampeni mjini
Kampala. Polisi walisema alijaribu kupitia
barabara isiyoruhusiwa.BONYEZA HAPA->https://twitter.com/AmamaMbabazi?ref_src=twsrc%5Egoogle%7Ctwcamp%5Eserp%7Ctwgr%5Eauthor
0 comments:
Post a Comment