Uongozi wa kampuni ya ACACIA inayomiliki migodo ya dhahabu
ya Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara imelalamikia changamoto ya kukatika umeme
mara kwa mara katika migodi yake huku wakilitaka shirika la ugavi wa umeme
Tanesco kufanya jitihada za haraka kutatua tatizo hilo ambalo limedumu kwa muda
mrefu na kuikosesha kuikosesha serikali mapato yakutosha.
Akizungumzia hali hiyo kaimu meneja uzalishaji katika mgodi
wa dhahabu wa Bulyanhulu Bw.Salvatory Tesha amedai hali ya upungufu wa umeme na
kukatika mara kwa mara imekua ikiisababishia kampuni ya ACACIA hasara huku mkuu wa wilaya ya Kahama Bw.Vitta Kawawa
akiuhakikishai uongozi wa kampuni ya acacia kuwa tatizo hilo litakwisha siku za
karibuni kwakuwa TANESCO inaendelea kujenga njia kubwa ya umeme kutoka singida
kupitia mkoa wa shinyanga.
Katika hatua nyingine mkurugenzi wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Bw.Graham Crew amekabidhi hundi ya zaidi ya shilingi milioni mia
saba kumi na nne na laki nane fedha ambayo ni sehemu ya koidi ya matumizi ya
ardhi kwa halmashauri ya msalala ambapo mkuu wa wilaya ya Kahama Bw.Vitta
Kawawa amewataka viongozi na watendaji wa halmashauri hiyo kusimamia na
kuhakikisha fedha hizo zinatumika
kujenga miradi ya maendeleo huku mkurugenzi wa halmashauri ya msalala
bw.patrick kalangwa akidai baadhi ya fedha hizo zitatumika kutatua changamoto
ya madawati katika shule za mzsngi na sekondari ili kutekeleza agizo la rais
John Pombe Magufuli.
0 comments:
Post a Comment