Wananchi wa kijiji cha ushiri Marangu wilaya ya Moshi mkoani
Kilimanjaro wamelalamikia askari wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa
kuwapiga na kudhalisha wanawake wanaingia katika hifadhi ya msitu wa mlima huo
kwa ajili ya kuokota kuni na kukata majani.
Wakizungumza wakati wa zoezi la kupanda miti katika kijiji
hicho
Kinachozunguka hifadhi ya mlima Kilimanjaro wananchi hao
wanasema adha wanayoipata ni kubwa na kwamba wameshawasilisha malalamiko yao
katika uongozi wa hifadhi hiyo bila mafanikiio.
Wanachi hao wamelazimika kuwasilisha kilio chao kwa mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro Aw.amos Makala na kusema kuwa mateso wanayoyapata wanawake
ni makubwa hali inayoondoa dhana ya ujirani mwema baina ya wananchi na uongozi
wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
Kufuatia malalamiko hayo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw.Amos
Makala amepiga marufuku askari wa hifadhi hiyo kunyanyasa wananchi na kuagiza uongozi wa Kinapa kuimarisha
mahusiano mazuri na wananchi wanaozunguka hifadhi ya mlima Kilimanjaro.
Kaimu mhifadhi mlima Kilimanjaro Bw.Charles Ngendo ameahidi
kutatua kero hiyo na kuimarisha ujirani mwema kwa kuanzisha na kusaidi miradi
ya Maendeleo.
0 comments:
Post a Comment