Waziri Mkuu wa zamani wa Uganda, Amama Mbabazi amesema
atakubali matokeo ya uchaguzi endapo kutakuweko uwazi katika mchakato mzima wa
kuhesabu kura.
Mbabazi ambaye aliwania urais kama mgombea binafsi kwenye
uchaguzi wa hapo jana alikuwa amesema hatayatambua matokeo ya uchaguzi na kudai
kwamba, chama tawala kimetumia hila na udanganyifu.
Hii ni katika hali ambayo, matokeo ya hivi punde
yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi yanaonyesha kuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani
ameshindwa kupata kura nyingi hata katika ngome yake ya nyumbani mjini Kanungu.
Habari za hivi punde zinaonyesha kuwa mgombea urais kwa
tiketi ya chama cha FDC, Kizza Besigye ameanza kumsogelea Rais Yoweri Museveni
aliyewania nafasi ya urais kwa tiketi ya NRM.
Hadi tunakwenda hewani Besigye alikuwa akishikilia nafasi ya
pili kwa asilimia 38 kwenye matokeo ya pili awali ambayo yametolewa asubuhi hii
na Tume ya Uchaguzi ya Uganda. Kwenye tangazo la kwanza,Besigye alikuwa na
asilimia 32 ya kura zilizokuwa zimehesabiwa wakati huo. Kwa sasa Rais Yoweri
Museveni bado anaongoza akiwa na zaidi ya kura milioni 1.3 sawa na asilimia
61.8.
0 comments:
Post a Comment