Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imerekodi
matukio 411 ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo kwa mwezi Januari.
Idadi hiyo imeongezeka kutoka ile ya mwezi Disemba ambapo
matukio 347 yalirekodiwa. Mikoa iliyoathirika zaidi ni ile ya mashariki mwa
nchi hiyo kama Kivu Kaskazini, Ituri, na Haut Uele.
Ripoti iliyotolewa na ofisi hiyo imesema, maofisa wa
serikali wakiwemo polisi, wanajeshi, idara za upelelezi, na mamlaka nyingine za
utawala zinahusika na matukio 274 yaliyoathiri watu 468.
0 comments:
Post a Comment