Serikali za Rwanda zimetangaza azma ya kuimarisha uhusiano
na ushirikiano wa pande mbili, kikanda na kimataifa na kuweka kando hitilafu
zilizolemaza muamala wa pande mbili hizo katika miaka ya hivi karibuni.
Ahadi hiyo imetolewa wakati wa mkutano kati ya Rais Paul
Kagame wa Rwanda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga mjini Kigali.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na Rais
Kagame, Waziri Mahiga amesema Tanzania imeamua kufungua ukurasa mpya wa
uhusiano na Rwanda kwa maslahi ya pande mbili na eneo zima la Afrika
Mashariki.
Mwanadiplomasia huyo wa Tanzania amesema mgogoro mashariki
mwa DRC, hali ya hivi sasa nchini Burundi pamoja na changamoto za kiusalama
katika eneo la Pembe ya Afrika vinahitaji ushirikiano wa kila nchi na kwamba
Rwanda ni nchi muhimu katika kukabiliana na changamoto hizo.
Rais Kagame kwa upande wake amesema Jumuiya ya Afrika
Mashariki haiwezi kufikia malengo yake endapo kutakuwa na hali ya kutoelewana
miongoni mwa nchi wanachama.
0 comments:
Post a Comment