Msemaji wa chama cha Forum for Democratic Change
Ssemujju Ibrahim Nganda amethibitisha kwamba mgombea urais wa chama hicho Dkt
Kizza Besigye aliyekuwa amekamatwa na polisi sasa ameachiliwa huru.
Kanali huyo mstaafu ambaye ni kigogo wa upinzani
nchini Uganda alikuwa amekamatwa katika kitongoji cha Naguru,mjini Kampala
katika nyumba ambayo upinzani ulidai wizi wa kura ulikuwa ukifanyika.
Wafuasi wa upinzani, wakiambatana na kanali Besigye,
wanadai walifumania watu wakiiba kura na wakataka usaidizi wa polisi kukagua
nyumba hiyo lakini wakazuiliwa.
Besigye alikamatwa na maafisa wa polisi walioondoka
naye kutoka eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment