Uchaguzi wa rais na bunge nchini Uganda ambao
ulianza saa moja asubuhi leo kwa saa za nchi hiyo katika vituo vingi vya kupiga
kura umemalizika saa moja jioni bila kuripotiwa visa vikubwa vya uhalifu na
uchakachuaji.
Mwenyeti wa Tume ya Uchaguzi Uganda, Badru Kiggundu
aliongeza muda wa kupiga kura kutoka saa kumi jioni ambao vituo vyote
vilitazamiwa viwe vimefungwa hadi saa moja jioni katika vituo ambavyo vilipokea
masanduku na makaratasi ya kupigia kura kwa kuchelewa.
Hadi tunaenda mitamboni zoezi la kuhesabu kura
lilikuwa linaendelea katika vituo vingi. Timu ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya
EU imesema kuwa asilimia 41 ya vituo vilipokea vifaa vya kupigia kura kwa
wakati na kwamba mpaka sasa zoezi hilo la kidemokrasia linaendelea
vizuri.
Wakati huo huo,Rais Yoweri Museveni ametetea hatua
ya kufungwa kwa mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter na Whatsapp
akisisitiza kuwa imetokana na sababu za kiusalama. Rais Museveni ambaye
ameongoza nchi hiyo kwa miongo mitatu sasa amesema kuwa wamechukua hatua hiyo
baada ya kuona baadhi ya wananchi wanatumia mitandao ya kijamii kueneza woga na
propaganda.
Mapema leo, Mkuu wa ujumbe wa AU, Sophia Okofor pia
amewataka raia wa Uganda kudumisha amani na kuwa watulivu baada ya
uchaguzi.
Wapigakura waliojiandikisha ni takriban milioni 15.3
na kuna vituo 28, 010 kote nchini Uganda. Wagombea urais ni wanane na kwa
upande wa bunge, viti vinavyowaniwa ni 290. Nafasi ya Urais imewavutia wagombea
8 akiwemo Rais Yoweri Museveni na Waziri Mkuu wa zamani, Amama Mbabazi pamoja
na mpinzani wa muda mrefu wa serikali, Dk. Kizza Besigye.
0 comments:
Post a Comment