Image
Image

Latest News:Matokeo kidato cha nne yatoka Ufaulu washuka kwa asilimia 67.91



Baraza la mitihani nchini Necta limetoa matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2015 kwa kutumia mfumo wa Division badala ya GPA ambapo ufaulu umeshuka kutoka asilimia 69.75 2014 hadi asilimia 67.91,2015.Kwa matokeo yote.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.
Msonde amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
Aidha kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.
Kwa upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.
Aidha waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.
Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.
Amesema kwa upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu wa juu kabisa ni wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 16.76 wamefaulu.
Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.BONYEZA HAPA->http://41.93.31.198/csee/matokeo/csee/2015/csee2015/index.htm
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment